Saturday, March 3, 2012

NAKUPENDAAAAAAAAAAAA

Kwenye maskani moja ya vijana hapa jijini hali haikuwa shwari kwa kijana mmoja kwani alikuwa mwenye huzuni kila wakati na hili lilitokana na wenzake kumcheka kila siku alipokwenda maskani hali hiyo ilitokana na kijana yule kutokuwa na msichana.Vijana wenzake baadaye wakagundua kuwa mwenzao tatizo lake kubwa ni aibu hivyo wakapanga kumsaidia ili naye apate demu.

siku moja wakiwa maskani,ghafla kwa mbali wakamuona msichana anakuja haraka sana wakamwambia mwenzao; “oyaa demu huyo anakuja inuka umfuatilie hatutaki ukae bila demu hapa.” Jamaa kwa upole akainuka na kumfuata yule demu mambo yakawa kama hivi :

Msichana: Sasa vipi mbona umenisimamisha halafu huniambii chochote?
Jamaa: Mimi naku...naku...nak...
Msichana: Sasa nitakuelewaje mbona humalizi maneno?
Jamaa: Naona aibu,tazama pembeni basi
Msichana: Wewe sema mimi nakusikiliza
Jamaa: Mimi wewe mimi na wewe... mimi...

Msichana: Mbona sikuelewi? Unanipotezea muda wangu ujue?
Jamaa,siyo hivyo,mwenzio naona aibu! nimekwambia angalia pembeni wewe hutaki!
Msichana: Haya basi nageuka ongea basi nikusikie.
Hapo hapo kabla hajaongea kitu yule jamaa,akaanza kutimua mbio huku akipayuka kwa sauti ya juu “Nakupendaaa,nakupendaaa!”
Wenzake kule maskani wakavunjika mbavu kwa kicheko.Courtesy : The GlobalPublishers