Saturday, March 3, 2012

KOFIA YANGU NIMEPEWA ZAWADI

Kuna babu mmoja toka Zanzibar alikuwa anasafiri katika meli toka Unguja kwenda Dar. Alikuwa amevalia kanzu kumbe huku ndani akiwa amevaa msuli na hakuwa na kufuli, kichwani alikuwa na kofia mpya. Kwa kuwa alikuwa amekaa mbele ya meli upepo wa bahari ulivuma na kuwafanya abiria wazuie vitu ambavyo vingeweza kupeperushwa na upepo. Yule babu alishikia kofia yake na kuacha kanzu na msuli vikipanda juu!
Baada ya upepo kutulia jirani yake alimuuliza:
“Mbona ulishika kofia na kuacha ikulu hadharani?”
“Kofia yangu nimepewa zawadi na leo ndiyo nimevaa, huku chini nimepata bure pia hapawezi kupeperuka na upepo.”
Majibu hayo yalimwacha hoi muulizaji. Mmh, kila mtu ana kitu chake anachokithamini.
Courtesy : The GlobalPublishers