Saturday, March 3, 2012

PANYA DUME

Akiwa amekaa kijiweni kwa muda mrefu bila kupata abiria, dereva teksi alishikwa na hali ya kutaka ‘kupumua’ hewa chafu hivyo kuamua kupumua kwa kuubanabana ndani ya gari yake huku milango ikiwa imefungwa. Alipomalizia kutoa hewa hiyo chafu, mteja akaingia na kukaa kwenye kiti akimtaka amuwahishe Kariakoo.
 
“Niwaishe Kariakoo mara moja.”
Wakati huo harufu ilikuwa kali kwenye gari hilo na baada ya mwendo mfupi abiria huyo alishindwa kuvumilia ikabidi aulize:
“Vipi mzee, kuna panya kafia humu?”


“Ndi..ndi..yo. “
“Tena panya mwenyewe dume na amekufa muda si mrefu.”
Kauli ile ilimfanya dereva anyamaze kimya. 


Courtesy : The GlobalPublishers