Friday, August 31, 2012

KWETU ZIPO TELE


Boti ilikua ikienda Zanzibar ndani yake kulikuwa na watu tofauti pamoja na mizigo yao, baada ya mwendo mrefu, Boti ikaanza kuzidiwa na mizigo na ikabidi mizigo ipunguzwe.

MZUNGU: Akatupa computer, akasema kwetu zipo tele.

MCHINA: Akatupa boksi la simu akasema kwetu zipo tele.

MHINDI:Akamwaga kiroba cha TAMBUU akasema kwetu zipo kibao.

MMASAI: Akatupa shanga akasema kwetu zipo nyingi.

 MCHAGA akawa anahaha hajui atupe nini,kila kitu chake alikionea uchungu, ghafla akamsukuma Mmasai akasema yesu na maria hawa wapo tele Arusha.