Tuesday, June 19, 2012

NIMEWASHA NJITI ZOTE MAMA



MTOTO mmoja alitoa kali ya mwaka baada ya kutumwa na mama yake aende dukani akununue kiberiti. Baada ya kurudi nyumbani, mama yake alimuuliza:
Mama: Umeisha nunua hicho kiberiti?
Mtoto: Ndiyo mama.


 
Mama: Umehakikisha ni kizima?
Mtoto: Ndiyo mama, nimezijaribu njiti zote zimewaka.
Mama: Haa! Mwanangu sasa tutawashia nini kama umewasha njiti zote?
Mtoto: Mama ningejuaje kama njiti ni nzima bila kuziwasha?
Mh! Mama alikosa cha kuzungumza akabaki kutikisa kichwa.



COURTESY: THE GLOBAL PUBLISHERS