Tuesday, June 19, 2012

STOPKijana mmoja aitwaye Charles, mkazi wa Yombo Dovya Dar, hivi karibuni alimpiga ‘stop’ mama yake mzazi asifike kwake baada ya kubaini anawagombanisha na mkewe.
Akiinyetishia safu hii ishu hiyo, jirani wa jamaa huyo alisema kuwa tangu alipooa ndoa yao ilitawaliwa na migogoro kila kukicha.


Jirani huyo aliongeza kuwa, kufuatia migogoro hiyo jamaa alikaa na mkewe ambaye alimweleza kila kitu kuhusu mama yake aliyekuwa akitoa maneno huku na kuyapeleka kule.
Habari zinapasha kwamba alipobaini chanzo cha matatizo alikuwa mama yake alimwita na kumwambia kama tabia yake ni hiyo ya uchonganishi, bora asifike kabisa nyumbani kwake.
“Kuinusuru ndoa yake jamaa alimpa laivu mama yake ambaye alijifanya kuja juu lakini mwanaye alisisitiza kama hataacha umbeya asifike kwake,” alisema shuhuda huyo.COURTESY: THE GLOBAL PUBLISHERS