Tuesday, June 19, 2012

SISTA-DUUUSistaduu mmoja aliyefahamika kwa jina la Zainabu, mkazi wa Temeke jijini Dar, hivi karibuni aliumbuliwa na mlio wa simu aliyoiba.
Habari kutoka kwa mpashaji wetu zinaeleza kwamba, dada huyo amekubuhu kwa wizi wa simu na fedha kwenye saluni mbalimbali.
Imeelezwa kuwa kwa jinsi alivyo mzuri na mcheshi huwezi ukamfikiria kama ni kibaka mzoefu.


“Siku aliyoumbuka aliingia kwenye saluni moja iliyopo mitaa ya Temeke Mwisho akaomba apakwe dawa kwenye nywele zake, msichana aliyekuwa akimhudumia alipotoka nje akaiba simu na kuiweka kwenye nguo yake ya ndani,” alisema shuhuda huyo.
Habari zinaongeza kuwa yule mhudumu alipogundua simu yake haipo alianza kulalamika lakini yule dada alitulia kimya hadi kaka mmoja alipoingia na kuipiga ndipo mlio ukatokea sehemu nyeti za yule dada ambaye alipewa mkong’oto wa kutosha.
COURTESY: THE GLOBAL PUBLISHERS