Wednesday, February 29, 2012

MAKOHOA MBAKA MAYAMBA


KUNA jamaa mmoja alikuwa akitembea na mke wa Mwarabu, muda alioutumia kukutana na mwanamke huyo ni pale mumewe alipokwenda kuswali msikitini ambapo dowezi huyo alikuwa akipita na kukohoa ndipo mke wa Mwarabu alitoka na kwenda kugawa utamu.

Wasamaria wema hawakurufahishwa na tabia za yule jamaa kumchukua mke wa mtu, ilibidi wamueleze mwenye mali mbinu alizotumia mgoni wake.

Mwarabu alipoelezwa hivyo, siku hiyo hakwenda msikitini alibana sehemu ili amkamate mwizi wa mali zake.
Mgoni alikuja kama kawaida akijua Mwarabu amekwenda msikitini, alikohoa kwa muda mrefu ndipo yule mwenye mali alimwambia;

“Leo makohoa mbaka mayamba mwenyewe nipo.”
Jamaa aliposikia hivyo akatoka nduki.Courtesy : The Globalpublishers