Wednesday, February 29, 2012

PICHA YA MVUA


MWALIMU wa somo la sanaa aliingia darasani na kuwaeleza wanafunzi wote wachore picha ya mvua inanyesha. Wanafunzi wote walichora picha ya aina hiyo kisha walikusanya madaftari, siku ya pili mwalimu alishangaa kukuta daftari moja limelowa maji.

Aliingia darasani akiwa ameshikilia daftari hilo na kuuliza:
Mwalimu: Nani mwenye daftari hili?
John: Mimi.

Mwalimu: Mbona daftari lako limeloa maji?”
“Mwalimu si ulisema tuchore picha ya mvua inanyesha kabla sijamaliza daftari lote lililoa na mvua.
Majibu ya Lyasi yalimwacha mwalimu amepigwa butwaa huku wanafunzi wakikauka kwa vicheko.


Courtesy : The Globalpublishers