Friday, December 14, 2012

KONDA HUYU KIBOKO


Msikie konda huyu;
MLOKOLE:konda toa nyimbo za dunia weka za yesu.
KONDA:samahani ndugu yesu mpka anaondoka hakuwahi kutoa albam
TOZI:humu ndani ya daladala kuna joto

KONDA:teremka ukapande friji
ABIRIA:konda kuna siti?
KONDA:waliokaa humu ndani wamekalia madumu?
SISTER DUU:konda unanibana
KONDA:hiyo suruali uliyovaa mbona inakubana hupigi kelele.
MAMA:sikai siti za nyuma.
KONDA:hizo siti za mwisho zipo nje ya gari au?