Monday, December 3, 2012

KIROBA CHA EMBE


Jamaa wawili waliiba kiroba cha Embe kisha wakakimbilia chumba cha kuhifadhiwa maiti na bila kujua wakati wanaingia wakaangusha Embe mbili mlangoni

 na mlinzi hakuwaona alikuawa amepitiwa na usingizi, aliposhtuka akasikia jamaa wanagawana hii yako hii yangu, Mlinzi akakimbia kumuita Daktari "njoo usikie malaika na shetani wanagawana maiti" walipofika mlangoni wakasikia "na zile mbili tulizoziacha mlangoni tukazichukue!" Daktari na Mlinzi mbio.