Thursday, January 10, 2013

BUSARA ZA MLEVI

Mlevi mmoja alioa mke ambae hajatulia hata kidogo. Siku moja mkewe akiwa na mwanaume mwingine nyumbani, mlevi akarudi home ghafla !! Mkewe akamwambia yule jamaa "usiondoke lala tu, mume wangu mlevi hatagundua". Jamaa akalala kweli, mlevi na yeye akapanda kitandani akalala !!

Baada ya muda kidogo mlevi akashtuka, akagundua tofauti hapo kitandani. Akahesabu miguu na kuona ipo sita akamshtua mkewe,. "Mke wangu mbona miguu ipo sita nani mwingine kalala hapa ?"
Mkewe akajibu kwa ukali "TOKA HAPA NA POMBE ZAKO, HEBU SHUKA KITANDANI UHESABU VIZURI!".

Mlevi akashuka na kahesabu...MOOJA......MBILI.....TAATU...NNE....Aaah kumbe kweli nilikosea kuhesabu, samahani sana mke wangu!!