Monday, January 14, 2013

TANGAZO


TANGAZO, TANGAZO Mtu mwenye watoto kumi atazawadiwa shilingi milioni 50.
Jamaa baada ya kusikia tangazo akamwambia mke wake "sisi tuna watoto tisa, ila nikuambie mke wangu mimi nina mtoto mmoja nje ya ndoa, naomba nikamchukue na huyo tupate hizo shilingi milioni 50. Mkewe akamwambia "poa." Jamaa akaenda kumfuata huyo mtoto, aliporudi hakuwaona wale watoto tisa akamuuliza mkewe "watoto wako wapi?" Mkewe akajibu " Baba zao walipoona tangazo nao wakaja kuchukua watoto wao. Jamaa akazimia.