Saturday, January 12, 2013

HEKA HEKA ZA UCHUMBA


Msichana mmoja alimpeleka mchumba wake kumtambulisha kwao,
alipofika tu baba akaona dosari maana kijana alikuwa mweusi tii, ana matege makali na kovu kubwa shavuni. Mchumba alipoona sura ya baba mkwe imebadilika ikabidi atabasamu kidogo, la haula! alikuwa na mapengo. Baba akaamua kumuita bintiye.
Baba: Mwanangu hebu twende nje tukaongee.
Binti: Baba seme hapa hapa mchumba wangu ni kiziwi.
Baba akazimia,