Tuesday, March 26, 2013

JARIBU KUWA KUKU


Kuna Daktari mmoja wa wagonjwa wa kichaa huko milembe alikuwa anawajaribu wagonjwa wake kama wamepata nafuu. Daktari akawaambia waannze kulia kama kama kuku. Wagonjwa wakaanza kulia wengine kama kuku jike wengine kama majogoo na wengine kama vifaranga. Daktari katika angalia yake akagundua kuna mgonjwa mmoja alikuwa amechuchumaa katika kona amekaa kimya halii kama kuku. Akaona afadhali amepata mgonjwa mmoja aliyepona. Akamfata yule mgonjwa na kumuuliza

Daktari: Mbona wewe haulii kama wenzio

Mgonjwa: Shiiiiih! nataga!