Tuesday, March 26, 2013

LOLIONDO



Rubani mmoja wa kigeni alikuja katika mbuga za Tanzania kwa ajili ya uwindaji nyama pori.

Akawaajiri wawindaji wawili akawapeleka kwa ndege hadi mbugani akawaacha wawinde ili akirudi na awachukue pamoja na nyama warudi mjini.
Aliporudi baada ya wiki moja akakuta wamewinda nyama nyingi kuliko uwezo wa ndege yake ndogo, rubani akaiangalia ile nyama kisha akawaambia “hatuwezi kuibeba nyama yote hii pamoja na nyinyi ndege itazidiwa uzito, itabidi nusu ya hiyo nyama tuiache”. Wawindaji wakasema “Mbona hata mwaka jana pia tulibebe nyama nyingi kama hii, na sisi wa wili na rubani aliyetuajiri katika ndege yenye uwezo kama wako, tuibebe tu”.

Rubani akasitasita lakini akaona awaamini akasema ” sawa haina tatizo, kama mlibeba mwaka jana basi tubebe tu na mwaka huu”

Wakapandisha nyama na wawindaji wakapanda kisha ndege ikaondoka, ilipofikia katika mlima wakaribu ndege ikashindwa kuenda juu zaidi kutokana na ule mzigo na hatimaye ikapata ajali katika mlima, kwa bahati nzuri wote walipata majeraha tu hawakufa.

Rubani: (huku akiwa ajielewi kidogo) Hapa tulipoangukia ni wapi?

Mwindaji mmoja: usijali, nahisi ni umbali wa mita 20 kutoka pale tulipoangukia mwaka jana

No comments:

Post a Comment