Thursday, November 22, 2012

MAMBA MWENYE HOFU

MAMBA
Siku moja hivi, Bibi alimtuma Toma mjukuu wake kwenda bwawani kuchota maji kwa ajili ya kupikia chakula cha usiku. Wakati Toma yuko bwawani anazamisha ndoo ili achote maji, akaona macho mawili makubwa yakimwangalia kwa makini. Kwa mshtuko akadondosha ndoo bwawani na kukimbilia nyumbani kwa bibi yake.
BIBI: “Enheee, ndoo na maji niliyokuagiza yako wapi?”
TOMA: “Mimi siwezi kuchota maji humo bwawani. Kuna Mamba mkubwa sana humo.”
BIBI: “Anhaaa!! ni hivyo kumbe? hata usimjali sana huyo Mamba. Amekuwemo humo bwawani miaka nenda rudi na hajawahi kumvamia mtu yeyote. Labda amekuogopa tu kama wewe ulivyomuogopa.”
TOMA: “Sasa, Bibi. Kama huyo Mamba ananiogopa kama na mimi nilivyomuogopa basi na hayo maji ya bwawani hayafai kwa kunywa.”