Friday, November 16, 2012

ZOBA NA GAZETIZoba alinunua gazeti akaingia nalo nyumbani kwa ujanja na kwenda kuliweka kwenye friji,
 Dada yake aliyekuwa sebuleni akifuma vitambaa akashangazwa na jambo hilo na kuamua kumuuliza Zoba “mbona umeweka gazeti ndani ya friji?” Zoba “wameandika gazeti lina habari moto moto hivyo nataka zipoe kidogo halafu ndio nizisome.”  Dada yake akabakia Aaaaaaaaah!!