Wednesday, November 21, 2012

MZAMIAJI

  MZAMIAJI
Jamaa mmoja alitoa kichekesho cha mwaka katika moja ya uzamiaji wake kwenye misiba kutoka Arusha, siku moja katika pitapita zake aliingia mtaa mmoja na katika kutembea kidogo akakutana na nyumba yenye msiba.

Jamaa akazamia kama kawaida yake na kwa bahati nzuri akakuta ndio waombolezaji waliokuwa wamekesha hapo walikuwa wanapata uji wa moto ili kufukuza baridi. Jamaa naye yumo akapata kikombe chake na kwa bahati mbaya akapaliwa na uji wa moto kiasi cha kutokwa na machozi. Wale wenzake msibani wakaaanza kumpa pole. Ili kupotezea kwamba hajaunguzwa na uji akaanza kusema (huku akionekana analia kwa sababu ya yale machozi) “MAREHEMU ALIKUWA MTU MZURI SANA” “YAANI ALIKUWA ANAPENDA WATU” “TAIFA LIMEPOTEZATUNU MUHIMU SANA” “MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI.” Waombolezaji “AAAhhhhhhhhh! Wazamiaji bwana.” Kumbe aliyekuwa anazikwa ni katoto ka siku moja tu!